Kim na Kanye watarajia mtoto wa nne

|
Kim Kardishian na Kanye West wakiwa na watoto wao watatu, wawili wakiwa wamezaliwa na Kim mwenyewe na mmoja akizaliwa kupitia mama mbadala

Kim Kardashian amethibitisha kuwa yeye na mumewe Kanye West wanatarajia kupata mtoto wao wa nne.

Kim ameweka wazi kuhusu wawili hao kutarajia kupata mtoto mwingine wa kiume kupitia kwa mama mbadala (surrogate mother) katika mahojiano na kituo cha Runinga cha Marekani.

Kim na mumewe Kanye tayari wamefanikiwa kupata watoto watatu ambao ni North, Saint na Chicago wenye umri kati ya miaka mitano na mwaka mmoja.  Mtoto Chicago pia alizaliwa na mama mbadala baada ya Kim kutahadharishwa na madaktari wake kuwa iwapo atabeba tena ujauzito huenda akahatarisha maisha yake.

Hata hivyo, familia yake Kim imepokea taarifa hizo kwa mshtuko licha ya kwamba hakuweka wazi lini mtoto huyo anatarajiwa kuzaliwa zaidi ya kusema "hivi karibuni".

Maisha
Maoni