Madonna ‘sina maisha' kama mama wa mcheza soka

|
Mwanamuziki Madonna akiwa na mwanaye David anayesomea masuala ya soka nchini Ureno

Mwanamuziki nyota wa muziki wa zamani, Madonna amesema kuwa mama mwenye mtoto anayeibukia kuwa nyota wa soka kumemfanya “kutokuwa na maisha", kutokana na mwanaye David wakati wote kuhitaji kuchukua kwaajili ya mechi tofauti.

Madonna amesema hayo hivi karibuni kuwa  "hana maisha " kwasababu ratiba ya kijana wake David Banda ya mechi kuwa ya mfululizo na hivyo kumfanya yeye pia kukosa muda.

Hivi karibuni Madonna na familia yake, walihamia mjini Lisbon, Ureno ili kumwezesha David kutimiza ndoto yake ya kuja kuwa nyota wa mpira wa soka.

Amesema, liko ya kukosa kufanya mambo mengi, lakini amekuwa akifurahia uamuzi wa kijana wake huo licha ya ratiba yake kuwa na mabadiliko ya mara kwa mara yanayosababisha na yeye “kubadili mipango yake."

Maisha
Maoni