Mbunifu wa vazi la harusi ya Meghan Markle bado ni siri

|
Prince Harry na Meghan Markle wakiwa katika maandalizi ya harusi yao mwezi ujao

Katika kuelekea siku kubwa inayosubiriwa kwa hamu na wananchi wa Uingereza na dunia ya kushuhudia mwana mfalme Prince Harry akifungana ndoa na mrembo kutoka Marekani, Meghan Markle, wengi wamekuwa na shauku ya kutaka kujua ni mbunifu gani atakayebahatika kumvalisha bibi harusi huyo mtarajiwa.

Mpaka sasa majina kadhaa ya wabunifu maarufu yamebashiriwa kuhusika na nguo hiyo lakini chanzo cha habari kwa mujibu wa Dailymail hata Prince Harry mwenwe hajafahamu nguo hiyo inafanyiwa kazi na mbunifu gani.

‘Amekuwa mtu wa mila kweli kweli na anataka suala hilo liwe la kushtukiza kwa siku hiyo,’ wamesema waliohojiwa ndani ya kasri la kifalme. 

Mbunifu wa vazi hilo la harusi la bi harusi Markle anatarajiwa kutangazwa na  Kensington Palace baada ya kuwasili kwenye kanisa la St George, Mei 19 na mlinzi wa siri. 

Mbunifu duo Ralph & Russo ambaye alishiriki kumtengenezea mrembo huyo vazi la usiku wake wa kutambulishwa rasmi akiwa na Prince Harry bado anapewa nafasi ya huenda ndiye anayeshughulikia nguo hiyo itakayovaliwa Mei 19.

Hakuna anayefahamu iwapo mbunifu Burberry amefanikiwa kupata fursa hiyo, lakini kwa mwaka huu inaonekana hakutakuwa na ubunifu kutoka kwa wabunifu wakubwa zaidi ya Meghan. ‘

Maisha
Maoni