Meryl Streep amtabiria mema Oprah Winfrey

|
Meryl Streep amtabiria mema Oprah Winfrey

Mcheza Filamu nyota maarufu nchini Markeani, Meryl Streep amesema, mjasiriamali maarufu na malkia wa vipindi vya Televisheni, Oprah Winfrey" anayo sauti ya kiuongozi", huku akimtabiria mwanamama huyo kuweza kuwania nafasi ya Urais.

Akirejea hotuba ya Oprah mwishoni mwa juma hili, aliyoitoa katika Tuzo za Golden Globes, Streep amemwambia mwandishi wa BBC, Andrew Marr kuwa "Hivi ndivyo namna watu wanavyoinuka. Hivi ndivyo unavyotakiwa kuongoza."

Mwigizaji huyo amesema,  amemsikia Oprah akisema "ni kweli amedhamiria kuingia katika kinyang’anyiro hicho.

Amesema Oprah "ameweka malengo ya juu kwa kila mmoja anayetaka kuingia katika kinyang’anyiro hicho" kwaajili ya urais 2020, aliongeza Streep.

Streep ni miongoni mwa washiriki waliokuwepo wakati  Winfrey alipozungumzia kashfa za kingono katika sherehe za tuzo Jumapili." Siku mpya imewasili katika mstari".

Maisha
Maoni