Mume wa Whitney Houston awashtaki BBC na Showtime

|
Marehemu Whitney Houston na Mwanaye Bobie Kristin enzi za uhai wao wakiwa na Bob Brown ambaye sasa amefungua kesi kulalamikia picha zao kurushwa na BBC na Showtime

Aliyekuwa mume wa mwanamuziki nyota wa Marekani, marehemu Whitney Houston,  Bobby Brown amekishitaki kituo cha runinga cha BBC na Showtime Networks kwa madai ya kutumia picha za video mwaka 2017 kama Makala iliyopewa jina la Whitney: Can I Be Me bila ridhaa ya wahusika.

Mashtaka hayo yamefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya jijini New York, Marekani jana Jumatano na Brown pamoja na wamiliki wa mali za binti yao Bobbi Kristina.

Mlalamika wa mashtaka hayo anadai kuwa, vipande hivyo vya video vimemuathiri yeye Brown, biashara yake pamoja na mali zinazomilikiwa na binti yake, Marehemu Bobbi Kristina.

Washtakiwa ambao ni Showtime, BBC na wakili wa Brown hawajasema chochote kuhusiana na kesi hiyo.

Mwanamuziki huyo wa R&B amesema dhima nzima ya kutumika kwa vipande hivyo vya picha za video haikupewa mtu yoyote kuitumia na kuongeza kuwa kazi hiyo ilipigwa miaka 15 iliyopita . Amesema picha hizo zilichukuliwa kabla ya wawili hao kuachana na marehemu Houston mwaka  2007 na kabla ya kifo chake mwaka 2012.

Mlalamikaji huyo amesema katika taarifa yake kuwa : "Kila mtu ni lazima awe na haki ya kudhibiti na kusimamia utambulisho wao au muonekano binafsi ama sauti au haiba yake katika biashara zinazofanywa na mwingine."

Filamu ama Makala hiyo inadaiwa kuwa ilioneshwa katika tamasha maarufu la Cannes mwaka uliopita na kisha kuoneshwa katika runinga za Showtime pamoja na BBC.

Mahakamani
Maoni