Polisi wapambana na waandamanaji Korea kusini

|
Waandamanaji Korea kusini wakipinga kuwasili kwa watumbuizaji na mashabiki wa michezo ya majira ya baridi wa Korea kaskazini katika bandari kuu ya nchi hiyo.

Kumetoka maandamano huko Korea Kusini muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Meli ya Korea Kaskazini katika bandari ya Mukho ikiwa na watu 140 wa kundi la sanaa.

Polisi wameonekana wakiwasukuma waandamanaji hao na kuleta tafrani ya aina yake bandarini hapo.

Nchi mbili majirani za Korea Kusini na Kaskazini zimekuwa zikifanya jitihada mbalimbali za kushirikiana hasa katika kipindi hiki cha michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ili kupunguza ukali wa mzozo baina yao kutokana na mipango ya Korea Kaskazini ya makombora ya nyuklia.

Mamia ya Polisi wenye ngao za kujikinga, walikuwa kwenye bandari hiyo kuzuia waandamanaji hao waliofika wakati wa kuwasili kwa meli hiyo huku wakipeperusha bendera ya nchi yao ya Korea kusini na ile ya Marekani na kuimba wimbo wa Taifa wa Korea Kusini.

Katika bendera hizo hakukuonekana bendera ya Umoja wa nchi hizo za Korea kama ilivyotarajiwa kufuatia makubaliano ya kubeba bendera moja kwenye ufunguzi wa michezo hiyo ya Olimpiki inayotarajiwa kufunguliwa Ijumaa, kama kuonesha kufikia hitimisho la uhasama wa miaka takribani 16.

Utawala
Maoni