Polisi yathibitisha kumshikilia 'Dudubaya' kwa mahojiano

|
Msanii Godfrey Tumaini maarufu Dudu Baya

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mussa Taibu amethibitisha kumshikilia Msanii Godfrey Tumaini maarufu Dudu Baya kwa matumizi mabaya ya mtandao.

Amesema tayari jalada limeshafunguliwa na uchunguzi unaendelea na endapo watajiridhisha kuwa ana hatia basi atafikishwa mahakamani muda wowote.

Dudu baya anaelezwa kujipeleka mwenyewe katika Kituo cha Polisi cha Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kukamatwa kwake kumetokana na maagizo ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akieleza kuwa Dudu Baya amemdhihaki marehemu Ruge Mutahaba.

Utawala
Maoni