R. Kelly afunguka kwa uchungu kuhusu tuhuma zinazomkabili

|
Mwanamuziki R. Kelly akizungumza kwa hisia kuhusiana na shutuma zinazomkabili wakati wa mahojiano na Kituo cha CBS Marekani

Mwanamuziki nguli wa muziki wa R&B nchini Marekani, R. Kelly ametoa machozi na kukanusha kwa hasira madai yanayomkabili kuhusiana na udhalilishaji wa kingono, ikiwa ni mahojiano yake ya kwanza tangu akamatwe mwezi uliopita.

Katika mahojiano yake yaliyokuwa yamejaa hisia kali, R.Kelly amesema, yeye siyo mpumbavu hadi afikie kufanya vitendo hivyo anavyodaiwa vya kuwashikilia wasichana wadogo bila ridhaa yao na kuwafunga kwa minyororo.

Amesema, amepitia mengi katika historia ya maisha yake, hivyo hawezi kufanya makosa ambayo yanaweza kumuharibia maisha yake ya sasa huku akisisitiza kamwe hawezi na ni ujinga unaoenezwa na mitandao.

"Sijafanya hivyo vitendo. Siyo mimi," alisema kupitia kipindi cha This Morning kinachorushwa na Kituo cha Runinga cha CBS cha Marekani na kuongeza kuwa "Ninapigania maisha yangu".

Amesema, yeyote anaweza kumpenda au kumchukia lakini hawezi kutenda vitendo hivyo anavyodaiwa kuvifanya.

Mwendesha mashtaka wa Chicago tangu tayari ameshamfungulia R. Kelly mashtaka 10 yakiwemo ya kudhalilisha kingono, akiwahusisha waathirika wanne wa madai ya vitendo hivyo, huku watatu wakiwa ni wenye umri mdogo.

Hata hivyo bado hajapatikana na hatia kutokana na mashtaka hayo na kwa sasa yuko nje kwa dhamana.

Iwapo atapatikana na hatia, R Kelly anaweza kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu hadi sba kwa kila kosa.

Maisha
Maoni