Rais Museveni hafahamu Kim Kardashian anafanya kazi gani

|
Kim Kardishian na mumewe Kanye West wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Yoweri Museveni Ikulu ya nchi hiyo, Kampala alipotembelea

Rais Yoweri Museveni wa Uganda jana alikutana na kufanya mazungumzo na nyota wa Muziki wa Rap, Kanye West aliyeambatana na mkewe Kim Kardashian.

Wawili hao mara baada ya kumtembelea Rais Museveni katika makazi yake jijini Kampala walimkabidhi zawadi ya raba za lebo ya Yeezy kwa lengo la kuweka kumbukumbu yao katika ziara hiyo.

Wakati wa mazungumzo yao yaliyolenga kuitangaza Uganda kupitia sekta ya Utalii, Rais Museveni alimuuliza mke wa Kanye anajishughulisha na nini kwaajili ya kujikimu na maisha.

Inadaiwa kuwa swali hilo lilitokana na malkia huyo wa kipindi cha maisha halisi cha runinga, mwenye miaka 37 aliyepo nchini humo kuonesha nia ya kutaka kumaliza haraka ziara hiyo.

'Walipokutana na Rais wa Uganda ndipo Rais alipomuuliza Kim, kwanini unataka kuondoka mapema,' moja ya chanzo kiliieleza Daily mail, na ndipo Kim alipomjibu nataka kurejea kazini.

'Rais akamuuliza tena, kazi gani unafanya na Kim, kwa upole akamjibu, anatengeneza shoo ya vipindi vya runinga na dada zake pamoja na familia na wote wanamsubiri yeye arudi.'

Maisha
Maoni