Rami Malek atwaa tuzo za Oscar kwa kumuigiza Freddie Mercury aliyezaliwa Z'bar

|
Raia wa Marekani mwenye asili ya Misri, Rami Malek aliyeshinda tuzo ya Oscar akimuigiza Freddie Mercury mzaliwa wa Zanzibar

Filamu ya Bohemian Rhapsody inayohusu maisha ya Freddie Mercury imefanya vizuri Tuzo za Oscar msimu huu kwa kuondoka na tuzo tatu huku kinara wa filamu hiyo, raia wa Marekani mwenye asili ya Misri, Rami Malek akishinda tuzo ya Muigizaji Bora wa Kiume.

Mercury aliyezaliwa Zanzibar alikuwa muimbaji mashuhuri wa Bendi ya Queen huku wimbo uliovuma zaidi ukiwa ni ule wa ‘We are Champions’

Filamu ya Bohemian Rhapsody imeshinda jumla ya Tuzo muhimu nne, huku filamu ya Roma na Panther pia nazo zikishinda tuzo tatu kila mmoja.

Maisha
Maoni