Ruby awamegea wenzake njia za kuwa maarufu mitandaoni

|
Mwanamuziki Ruby

Kufuatia sakata la baadhi ya wasanii kukumbwa na rungu la serikali kwa makosa ya kukiuka maadili ya jamii ya kupiga picha za utupu na kuzitupia mitandaoni, mwanamuziki wa bongo fleva aliyetamba na kibao cha 'Na Yule' Ruby amewapa mbinu mpya wasanii wenzake wanataka kupata umaarufu huo na kuwashauri kuwa zipo njia nyingi za kuweza kufikia umaarufu huo.

Amesema, umaarufu haupatikani kwa kupiga picha za utupu au kudhalilishana, badala yake watumie njia aliyofanya yeye ya kutengeneza umbo lake.

Ruby ameyasema hayo, wakati akijibu maswali kuhusu kuweka picha mtandaoni zilizosababisha utata wa umbo lake tofauti na alivyozoeleka.

Ruby amesema kwamba kupitia simu msanii anaweza kujiremba kwa jinsi ambavyo anataka na hivyo kuweza kusababisha mashabiki zake waendelee kumfuatilia na hata kumjadili.

"Zile picha zenye kunionyesha umbo kwanza alinitengenezea shabiki yangu akanitumia kisha mimi nikaona niiweke mtandaoni kama somo kwa wasanii wenzangu. Unaweza kufanya kitu kama kile na ukapata ‘attention’ uliyokuwa unaitaka. Badala ya kupiga picha za utupu wakati kwa sasa serikali iko macho siyo vizuri. Napenda tuwe wabunifu" amesema Rubby..

Muziki
Maoni