Wasanii miongoni mwa wajumbe wa bodi BASATA

|
Wasanii wa muziki na Bongo fleva (kushoto) Single Mtambalike maarufu Richie na Hamis Mwinjuma (kulia)

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amewateua wajunbe wapya wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa BASATA siku chache baada ya Rais Magufuli kumteua Mwenyekiti mpya wa Bodi hiyo, Habbi Gunze.

Miongoni mwa walioteuliwa ni mwanamuziki Hamis Mwinjuma maarufu 'MwanaFA'  pamoja na Msanii wa filamu, Single Mtambalike maarufu kama 'Richie'.

Wengine walioteuliwa ni pamoja na Asha Mshana, Mwadhiri msaidizi Sanaa UDOM, Dkt. Emmanuel Ishengoma wa Mnadhiri wa Chuo Kikuu Dodoma, Dkt. Saudin Mwakaje mwadhiri Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Uteuzi huo umeanza rasmi tangu Oktoba 5 na watatumikia kwa miaka mitatu.

Utawala
Maoni