Yvonne asema hajutii kuzaa nje ya ndoa

|
Mwigizaji Yvonne Nelson wa Nigeria na mzazi mwenzie Roberts

Mwigizaji maarufu wa Filamu za Kinigeria, Yvonne Nelson amesema hajutii kuzama binti yake nje ya ndoa.

Yvonne alimkaribisha mtoto wake wa  kwanza wa kike Ryn Roberts, Jumapili ya Oktoba 29 mwaka jana na  mchumba wake, Jamie Roberts.

Hivi karibuni akiwa katika mahojiano na BBC, Yvonne alisema, ingawa anaamini kupata mtoto ndani ya ndoa ni kitu kizuri, hajutii kuitunza mimba yake na kujifungua binti yake huyo.

“Naamini ni kitu kizuri nilichofanya. Kufunga ndoa, kupata watoto, kuwalea watoto katika familia ni jambo zuri lakini naamini jamii za Kiafrika zimekuwa zikituletea shinikizo kubwa mno kwa wanawake na wasichana .”

Alipoulizwa anajisikiaje watu wanavyomkosoa baada ya kupata binti yake huyo, Yvonne amesema

”Mimi ni mtu ninayechukulia mambo kwa chanya sana. Siruhusu vitu vya kunirudisha nyuma au kunizungumzia vibaya viniathiri. Nilibaki chanya wakati wote. Nilikuwa na watu waliokuwa wakinipenda wakati wote jumlisha Baraka hii nzuri mikononi mwangu. Ilikuwa furaha yangu katika kila kona. Sikuwa nasikiliza mambo mabaya kutoka nje. Hakuna kilichoniathiri kabisa”

Kwa mujibu wa nyota huyo alisema, kikubwa anachojali ni kuwa “mwisho wa siku kama mama yangu na familia yangu wananifurahia, hiyo ndiyo huwa furaha yangu pia”.

Filamu
Maoni