Test
Angelina Jolie mwigizaji aliyepitia tamu na chungu nyingi maishani

Angelina Jolie ni muigizaji anayeongoza katika tasnia ya filamu Marekani “Hollywood” alijipatia umaarufu mwingi katika filamu nyingi zikiwemo za Mr and Mrs, ‘Salt’ na ‘Maleficent’.

Angelina Jolie alizaliwa Juni 4, 1975, Los Angeles, California katika familia ya Jon Voight na Marcheline Bertrand.

Alianza kuigiza akiwa na umri mdogo. Alisoma Lee Strasberg taasisi ya Cinema akiwa kijana na baadaye alijiunga na Chuo cha uigizaji cha New York.

Alianza kuigiza mwaka 1997  kama mwigizaji msaidizi katika filamu ya ‘First Lady of Alabama Cornelia Wallace’ na kupata tuzo ya mwigizaji bora msaidizi katika tuzo za Academy pia Jolie alifanikiwa kufanya vizuri na kupewa nafasi katika filamu ya ‘Gia’ iliyozungumzia maisha ya taabu na ya kuhuzunisha ya mwanamitindo nguli Gia Marie Carangi na kujinyakulia tuzo ya

Angelina Jolie ambaye mwaka 2001 alichaguliwa kuwa Balozi wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa alitangaza kazi yake hiyo kwaajili ya kupata msaada wa wakimbizi huko Cambodia, Darfur na Jordan.

Jolie mpaka sasa ameshaolewa mara tatu. Mwaka 1995 aliolewa na nyota mwenzake katika ulimwengu wa filamu, Jonny Lee Miller.

Wanandoa hao waliachana mwaka 1999. Mwaka uliofuata aliolewa na mwigizaji Billy, Bob Thornton, ndoa hiyo ilidumu mpaka mwaka 2003, na kuachana. Wakati filamu ya Mr and Mrs Smith inatengenezwa Jolie alikutana na mumewe waliyeachana Brad Pitt.

Mwaka 2002, Jolie alimuasili mtoto wa kiume kutoka Cambodia na kumuita Maddox, baada ya miaka mitatu alimuasili mtoto wa kike Zahara.

2006 mtoto wao wa kwanza Shiloh alizaliwa nchini Namibia. Mwaka 2007, Angelina Jolie alimuasili kijana wa kiume mwenye miaka mitatu katika Kituo cha Yatima Vietnam na kumuita Pax Thien.

Jolie alizaa mapacha Knox Leon na  Vivienne Marcheline 2008 kusini mwa Ufaransa.

Kabla ya kupata watoto wake hao mwaka 2007, nyota huyo alipatwa na pigo kubwa la kumpoteza mama yake mzazi. Kifo chake kilitokana na saratani ya kizazi. Bibi yake pia alikufa na ugonjwa huo huo.

Mei 2013 nyota huyo alitangaza kwenye gazeti la New York Times taarifa iliyobeba kichwa cha habari “My Medical Choice” baada ya kufanyiwa upasuaji mara mbili ili kuzuia saratani ya matiti.

Muigizaji huyo alisema aliamua kufanya upasuaji huo baada ya kujua ana jinsi zinazojulikana kwa jina la BRCA1.

Mnamo Septemba 2016, Angelina Jolie aliachana na mume wake Brat Pitt.

Paul Pogba anaposikitikia mashambulizi ya mara kwa mara Uingereza

Nyota wa Manchester  United, Paul Pogba amelezea masikitiko yake makubwa kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara yanayofanywa nchini Uingereza.

Nyota huyo amenukuliwa akisema ni lazima  namna ifanyike ili kukabiliana na tatizo hilo: “Hatuwezi kuruhusu mashambulizi ya mabomu yaharibu maisha yetu.” Paul Pogba

Nyota huyo wa mpira wa miguu anayechezea klabu ya Manchester Utd, amefunguka na kuelezea  ugumu wa maisha unaowakabili kama waislam katika mji wa Manchester baada ya shambulizi la bomu katika mji huo mwezi uliopita,  huku akisisitiza kuwa magaidi wasipewe nafasi ya kushinda.

Katika mahojiano ya jarida la Julai / Agosti la  Esquire, nyota huyo wa Manchester United pia aliongelea kifo cha baba yake Fassou akiwa na umri wa miaka 79 kilichotokea hivi karibuni.

Nyota huyo aliyenunuliwa kwa dau kubwa amefanikiwa kukiongoza kikosi cha Timu yake kunyakua ushindi wa Ligi ya Uingereza, Mei 24 siku mbili baada ya mashambulizi yaliyotokea jijini Manchester na kuua watu ishirini na wawili na  kujeruhi wengine baada ya Tamasha la mwanamuziki Ariana Grande.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 raia wa Ufaransa alisema ushindi wa timu yake katika Ligi ya Uingereza ni kwaajili ya waathirika na anaamini mashambulizi ya huko London - hayana uhusiano na dini.

Pogba, ambaye amefanikiwa kwenda kutembelea msikiti mtakatifu huko Makka mwishoni mwa msimu, amesema: 'Kipindi cha mashambulizi ni kigumu sana lakini huwezi kuacha. Hatuwezi kuwaacha kuingia katika vichwa vyetu - tunapaswa kupigana.’


“Mambo ya kusikitisha yanatokea katika maisha lakini huwezi kuacha kuishi.” Huwezi kuua mwanadamu. Kumwua mwanadamu - si kitu kizuri, kwa hivyo sitaki kuweka dini juu yake, akaongezea na kusema 'Hii siyo Uislamu na kila mtu anajua hiyo. Mimi sio peke yangu ninayesema hivyo.’

Tangu kuhamia Manchester kutoka Juventus kwa lengo la kuvunja rekodi ya dunia, Pogba anajulikana kwa tabia yake ya upendo, kucheza na mitindo ya nywele zenye rangi. Anasema kuwa kifo cha baba yake kilichotokea wiki mbili kabla ya fainali huko Stockholm kilimkumbusha kwamba ni wajibu kufurahia maisha.

Unapopoteza mtu unayempenda, huwezi kufikiri sawa, "aliongeza. 'Ndiyo sababu nasema ninafurahia maisha, kwa sababu maisha ni mafupi. Nakumbuka nilipokuwa nazungumza na baba yangu na sasa hayuko hapa. Alikuwa mtu mwenye nguvu sana, mkaidi pia. Alipigana, lakini kwa umri wake haikua rahisi.” baba yangu alikua mtu mzuri sana, baba mzuri na ninafurahi kuwa mwanawe."

Pia alisema katika msimu uliopita, walinyakua tuzo tatu chini ya Jose Mourinho katika msimu wa kwanza wa meneja huyo wa Old Trafford kama haki kwa wachezaji.

'Nakubali kwamba hatukucheza vizuri, hatukufanya hivi, hatukufanya vile,' alisema.

'Unaweza kuwa timu bora duniani, unaweza kucheza soka kubwa na kushinda tuzo sifuri. Na ni nani anayekumbuka? Hakuna mtu.

Klabu hiyo awali ilijipatia pauni 800,000 kwaajili ya kumtoa Pogba alipoondoka kutafuta fursa kwa timu ya Juventus mwaka 2012.

Anasisitiza kuwa alikuwa na hamu ya kucheza mpira wa miguu ambayo imemsababisha kuondoka kwa matakwa ya Sir Alex Ferguson na anakubali kwamba hakuweza kuelewa lafudhi ya kocha huyo wa awali wa United wakati alipokuja kutoka Ufaransa akiwa na umri wa miaka kumi na sita.

“Mara ya kwanza, sikuweza hata kuelewa wachezaji wenzangu na lafudhi zao za Mancunian, "alisema . Marafiki zangu, walinicheka. Wakasema, "Oh, unakumbuka siku za mwanzo ambazo ulishindwa kuzungumza na sasa – unaongea lafudhi ya Mancunian."

'Nilienda Manchester kucheza soka. Hayo ndiyo yote niliyoyataka. Ingawa nilikuwa mdogo, nilihisi ningeweza kucheza, lakini sasa sitaki kusubiri", alisema mwanasoka huyo.

 

Afrika kusini yapiga marufuku dini katika shule za Umma

Mahakama Kuu ya kusini mwa mji wa Gauteng nchini Afrika kusini imezitangazia shule za umma kutojihusisha na masuala ya dini yoyote.

Suala hilo limekuja kufuatia taasisi ya Elimu ya dini na demokrasia kuwasilisha kesi  iliyofunguliwa dhidi ya shule sita zenye kusimamia tamaduni za Kikristu.

Katika maombi yao waliyoyawasilisha mahakamani hapo, taasisi hiyo inapinga uamuzi wa shule hizo kuzuia mafunzo ya sayansi katika dhana ya mageuzi ikisema ni ukiukwaji wa haki za watoto hao.

Akikabidhi hukumu ya kesi yao, Jaji Willem van Der Linde alisema, mahakama hiyo imezingatia suala la imani moja inayopaswa kutangazwa shuleni.

Kwa hukumu hiyo, shule za umma zinawajibu wa kuangalia upya sera zake zinazohusu masuala ya dini.

 

Mosul washeherekea Eid baada ya miaka mingi bila IS

Watu wa nchini Iraqi katika mji wa Mosul jana walishehereka Sikukuu yao ya kwanza ya Eid  bila uwepo wa Kundi la Islamic State katika kipindi cha miaka kadhaa baada ya wapiganaji hao kuondolewa katika eneo kubwa la mji huo na kuwepo kwa matumaini ya kukombolewa kwa eneo lililosalia katika mapigano yanayoendela,

Watoto walikusanyika katika eneo lao la kuchezea huko upande wa mashariki ya mji.  Wengine walicheza katika bembea za zamani, bunduki bandia ambazo ziliruhusiwa kuwa miongoni mwa michezo na wapiganaji wa IS baada ya kuutwaa mji huo Juni 2014.

Wapiganaji hao walianzisha utaratibu wa kuweka midoli yenye sura walizozihusisha na ibada za sanamu, na kuhamasisha vijana kujifunza matumizi ya silaha sanjari na kubadilisha vitabu kuakisi itikadi zao za kijeshi.Pia katika somo la hesabu walihimizwa kujifunza namna ya kuongeza mabomu na risasi.

Ibada za Idd hazikuruhusiwa chini ya utawala wa Islamic State lakini sherehe nyingine ziliruhusiwa.

Sakaya aitaka Serikali iweke ukomo wa uzazi

Mbunge wa Kaliua mkoani Tabora, Magdalena Sakaya ameitaka Serikali kuweka ukomo wa idadi ya watoto ili kuendana na uwezo wa serikali wa kupeleka huduma muhimu na maendeleo kwa wananchi kikamilifu.

Sakaya ametoa pendekezo hilo bungeni mjini Dodoma, katika swali lake kuhusu mpango wa serikali katika kudhibiti kasi ya ongezeko la watu nchini, swali lililojibiwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji.

Katika majibu yake, Dkt. Kijaji amesema serikali haiwezi kuweka ukomo wa idadi ya watoto kwa kuwa suala hilo ni kinyume na utamaduni na pia haliihusu serikali pekee, bali jamii nzima.

"Suala hili ni suala mtambuka na ni suala la kijamii, hivyo kusema serikali itoe tamko haitakuwa sahihi kijamii na kitamaduni zetu."

Akizungumzia sababu ya kasi ya ongezeko la watu kwa Tanzania, amesema sababu kubwa ni vizazi au idadi kubwa ya watoto ambao kina mama hujifungua katika maisha yao huku akitaja ukosefu wa elimu kuwa ndiyo chanzo kikubwa cha kina mama wa kitanzania kuzaa watoto wengi.

"Tafiti zinaonyesha kuwa kina mama wenye elimu ya kuanzia sekondari na kuendelea huzaa watoto wachache zaidi ikilinganishwa na wanawake wasio na elimu au wenye elimu ya msingi, wasichana au kina mama wenye elimu wanakuwa na uelewa mpana zaidi kuhusu njia za kisasa za uzazi wa mpango, madhara ya mimba za utotoni, madhara ya kuzaa watoto wengi pamoja na madhara hasi kwa baadhi ya mila potofu."

Hata hivyo, Naibu Waziri Kijaji amesema Serikali ya Tanzania ina sera ya kudhibiti idadi ya watu ya mwaka 1992 ambapo pamoja na mambo mengine inasisitiza utoaji wa elimu kwa watoto wa kike jambo ambalo linatekelezwa hivi sasa kupitia sera ya elimu bila malipo, kwa kuzingatia ukweli kuwa mtoto wa kike akipata fursa ya kukaa shuleni muda mrefu hataweza kuzaa watoto wengi.

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, kasi ya ongezeko la idadi watu nchini ni asilimia 2.7 huku wastani wa kiwango cha uzazi cha watoto katika familia ikiwa ni watoto watano kwa kila mwanamke mwenye umri wa kuzaa ambao ni miaka 15 hadi 49.

Luis Suarez amwaga machozi ya furaha

Mara baada ya kutua katika uwanja wake wa kwanza katika mchezo wa Soka, mchezaji  wa Luis Suarez alimwaga machozi mbele ya umati wa mashabiki wa  Klabu  ya Nacional nchini Uruguay waliofika kumlaki kwa heshima.

Mchezaji huyo nyota wa Timu ya Barcelona alimwaga machozi  kwa hisia baada ya kushuhudia umati wa mashabiki wa klabu yake hiyo wakimshangilia baada ya kurejea katika uwanja huo ambao ndio wenye historia ya kumbukumbu zake muhimu katika ulimwengu wa  soka.

Nyota huyo na Familia yake walitembelea klabuni hapo  baada ya kurejea nyumbani kwa mapumziko na kukaribishwa kwa heshima sanjari na kuzindua Sehemu mpya ya uwanja uliandikwa jina lake kama ishara ya Heshima.

Katika uzunduzi huo wa Jengo na Kituo cha Mafunzo cha Luis Alberto Suarez katika Uwanja wa Nacional's Los Cespedes mjini Montevideo, mchezaji huyo alionyesha furaha yake ya wazi iliyopelekea kushindwa kujizuia kumwaga machozi hayo.

Akizungumza baada ya kupata nafasi alisema, amefurahishwa na heshima aliyopewa.

"Namshukuru Mke wangu kwa mchango wake alionipa katika kipindi chote cha miaka 13 ya  ndoa yetu, hili ni jambo la kupendeza na ilikuwa ndoto yangu ili wanangu waje kushuhudia jambo hili." 

Kevin Hart: Kutoka kuuza duka hadi mchekeshaji maarufu duniani

Kutoka mchekeshaji maalum wa vipindi hadi Mcheza filamu kiongozi na mwenye jina kubwa katika kuongoza hafla mbalimbali, si mwingine tunayemzungumzia hapa ni, Kevin Hart ambaye ana kila uwezo wa kukuvutia katika masuala ya vichekesho.

Amezaliwa na kukulia katika mji wa Philadelphia, Hart alianza kuwa na ndoto za kuwa mchekeshaji tangu akiwa mfanyakazi wa duka la kuuza viatu.

Baada ya kujenga uwezo wake wa kujiamini katika maonyesho ya usiku , aliachana na kazi yake ya mchana na kuanza kutimiza ndoto zake katika klabu maarufu kama ya Caroline na The Comedy Store.

Baadaye kazi ya kutengeneza filamu ilifuata, akacheza filamu kama  Paper Planes na Scary Movie 3.

Akatengeneza filamu ambayo yeye  Hart alikuwa mwandishi na mchezaji kiongozi katika  mchezo ulioonyeshwa kwenye runinga ya ABC  iliyojulikana kama The Big House katika mwaka 2004.

Katika nafasi yake ya mchezaji kiongozi kwenye filamu ya Soul Plane  sanjari na vichekesho vyake maalumu  ni miongoni mwa kazi ambazo hutachoka kuziangalia.

Katika Makala yake ndefu iliyopewa jina la, Laugh At My Pain, Hart aliweka rekodi  ya kufanya vizuri katika kundi la vipindi.

Hart amekuwa mmoja wa baadhi ya wachezaji wanaofanya vizuri katika fani ya filamu kwenye miaka michache iliyopita ikiwemo ile ya Think Like a Man, Get Hart, Ride Along na The Wedding Ringer.

Katika mwaka 2015, alitunukiwa tuzo ya mchekeshaji halisi wa MTV.  Hart pia aliweka historia ya kipekee katika ziara yake ya hivi karibuni iliyoitwa , What Now?  Sanjari na kung’ara katika nyimbo za BET kupitia vipindi vya Real Husbands of Hollywood

Akiichukulia kwa umuhimu nafasi yake ya ujasiriamali , Kevin Hart  anajiandaa kutoa kitabu kitachoelezea Maisha na mahangaiko yake kwa jumla. Kwa mujibu wa ukurasa wa sita wa kitabu hicho chenye jina la  Ride Along star, alichoshirikiana na Atria Publishing Group kinazungumzia mafanikio sanjari na matarajio yake.