Test
MWANGALIZI WA WANYAMA ASHAMBULIWA NA CHUI HADI KUFA, NI CHUI ALIYEMPENDA SANA

Salamu za pole za heshima zimeendelea zikimiminika kufuatia ajali mbali ya kuraruliwa hadi kufa kwa mwangalizi wa hifadhi ya wanyama aliyeuawa kwa kushambuliwa na chui aliyempenda wakati akifanya jitihada za kumsaidia mwenzake.

Rosa King,aliyekuwa na miaka  33, alifariki dunia baada ya kushambuliwa na chui huyo katika hifadhi ya wanyama ya Hamerton huko Cambridgeshire.

Mama wa Rosa, Adrea akizungumza kwa majonzi, amesema mototo wake aliyatoa maisha yake katika kazi hiyo, ' asingeweza kufanya chochote kile, ni hiki tu alichokuwa akikifanya, na ndicho alichopenda kukifanya.'

Marafiki na wafanyakazi wenzake wamemuelezea Rosa kama taa iliyowaka, katika kuleta mvuto na kuongeza kuwa alikuwa HIFADHI'.

Mashuhuda wamesema, walisikia kelele za kutisha, kutoka katika eneo lililofungwa, huku wageni zaidi ya 100 wakiondolewa sanjari na kuwepo kwa mtafaruku na uvumi wa kwamba chui ametoroka. 

Mwanadada huyo aliyekuwa na miaka 33 inadaiwa alikuwa akifanya jitihada za kumuokoa mwenzake kwa kutupia chui huyo mafungu ya nyama ili kumvuruga, alisema shuhuda

Msimamizi wa usalama wa Cambridgeshire,  amethibitisha kutodhuriwa kwa chui huyo lakini amesema, uchunguzi  unafanyika chini ya mamlaka ya leseni ya Halmashauri ya Wilaya ya Huntingdonshire. 

Uvumi umesambaa katika mitandao ya kijamii, ikidai mnyama huyo ameuawa, licha ya  mamlaka hiyo kutothibitisha ni hatua gani itazichukua kwa chui huyo.