Acacia North Mara sasa kulipa fidia ya ardhi wananchi 203.

|
Baadhi ya maeneo ambayo yanatarajiwa kulipwa fidia na mgodi wa Acacia North Mara

Mgodi wa Acacia North Mara kesho, Jumatatu Machi 04, wanatarajiwa kuanza kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi 203 wa vijiji vya Nyabichune, Mji Kati, Nyangoto na Nyakunguru  yenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.8.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Acacia iliyotumwa kwa vyombo vya habari leo, Machi 03, wanufaika hao ni wale wananchi waliofanyika tathmini ya 20 ya mwaka 2011 – 2012 pamoja na awamu ya 35,41 na 42.

Aidha uongozi wa ACACIA North Mara umewataka wananchi wa Nyabichune wa maeneo ya Makerero waliofanyiwa tathimini katika awamu ya 47 kufika kesho, Jumatatu pia kuchukua fidia zao.

Taarifa hiyo pia imesema, watakaolipwa fidia hiyo ni wale wote ambao ni wakazi halisi wa maeneo yaliyochukuliwa taarifa zao na mgodi na kwamba orodha kamili  ya wahusika wote imekabidhiwa kwa viongozi wa vijiji na vitongoji husika.

Meneja wa Idara ya Jamii Endelevu wa Mgodi huo, Richard Ojendo amesema mgodi huo umechelewa kufanya zoezi hilo kutokana na watu wengi kutokuwa na uhalali wa umiliki wa maeneo hayo.

Amesema zoezi hilo litafanyika kwa siku tano katika Ofisi za Jamii za mgodi huo na kusema wananchi wataohusika ni wale waliofanyiwa tathimini huku wengine wakitakiwa kuwa na subira.

Fedha
Maoni