Agizo la Rais Magufuli latekelezwa, mafuta yaanza kutoka bandarini

|
MOja ya gari lililobeba mafuta tayari kwa kusafirishwa sehemu mbalimbali

Agizo la Rais, John Magufuli la kuachiwa mafuta yaliyokuwa yanashikiliwa Bandarini  Dar Es Salaam, limeanza kutekelezwa ambapo malori yaliyobeba bidhaa hiyo yalionekana yakitoka bandarini kwenda kwenye viwanda vinavyoyamiliki.

Tukio hilo limeshuhudiwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ambaye amewatoa hofu Watanzania kwamba mafuta ni ya kutosha kwa muda wote, huku akitaka Mamlaka zinazoshikilia mafuta hayo ziyaachie kwa utaratibu.

Wafanyakazi kwa upande wao wanaendelea kuchapakazi ambapo baada ya kujionea haya Waziri Mwijage amewataka wananchi kutokuwa na hofu kuhusu upatikanaji wa mafuta na kuahidi kutembelea viwanda vyote.

Kwa mujibu wa Mwijage shughuli ya uzalishaji wa mafuta ya kupikia itafanyika usiku na mchana ili kuondokana na uhaba wa mafuta uliokuwa unadaiwa upo katika baadhi ya maeneo.

Chakula
Maoni