ANAISHI KWA KULA MAFUTA, SUKARI NA MAZIWA

|
Kijana wa Miaka 15 anayedaiwa kuishi kwa kula maziwa, mafuta na sukari kila siku huko Tunduru

TUNDURU….TANZANIA

 Katika hali ya kustaajabisha, Mwanafunzi SHUKURU MUSSA KISONGA mwenye umri wa miaka 15 wa Shule ya Sekondari ya MGOMBA, Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, hadithi ya maisha yake imekuwa ni ya kusimumua  kufuatia mwili wake kutohitaji chakula cha aina yeyote zaidi ya Mafuta ya kula, Sukari pamoja na Maziwa.

 SHUKURU KISONGA hutumia Mafuta ya kula na maziwa kiasi cha Nusu Lita pamoja na Sukari Nusu Kilo kila siku iitwayo leo, na endapo akikosa vyakula hivyo mwili wake hubadilikabadilika rangi na macho huongezeka ukubwa.

Maisha
Maoni