Angelina Jolie atembelea wakimbizi wa Rohingya

|
Angelina Jolie akiwasili katika kambi za wakimbiza wa Kiislamu kutoka Rohingya kama mjumbe maalum wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia wakimbizi

Mcheza filamu nyota wa Hollywood nchini Marekani, Angelina Jolie ametembela kambi ya wakimbizi wa Rohingya iliyopo nchini Bangladesh jana Jumatatu ikiwa ni kuelekea utekelezaji wa ahadi mpya ya Umoja wa Mataifa ya kutumia takribani dola za Kimarekani bilioni moja kwa ajili ya kuwahudumia wakimbizi hao.

Baada ya kuwasili kusini mwa Taifa hilo la Asia, Jolie ambaye ni mjumbe maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi la UNHCR, alikwenda moja kwa moja katika kambi ya Teknaf iliyopo karibu na mpaka wa Myanmar na kuzungumza na baadhi ya Wakimbizi 720,000 wa Kiislam walikimbia mahambulizi kutoka kwa vikosi vya jeshi Agosti 2017.

Katika ziara hiyo Jolie mwenye umri wa miaka 43 hakutangaza ahadi yoyote, lakini Naibu mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ikbal , Hossain ameieleza AFP kuwa Jolie ameahidi kutembelea kambi nyingine zaidi leo, Jumanne.

Maisha
Maoni