Baba adaiwa kumbaka mtoto wake wa miaka minne

|
Tuhuma za ubakaji

Mtoto mwenye umri wa miaka minne anadaiwa kubakwa na Baba yake Mzazi mwenye umri wa miaka 35 anayeishi  mtaa wa Nyankumbu Halmashauri ya Mji Geita.

Taarifa zinasema kuwa Baba huyo alikuwa akiishi na watoto wake wawili akiwemo huyo aliyedaiwa kumbaka  baada ya kuvunjika kwa ndoa yake na mama wa watoto hao.

Akisimulia tukio hilo, mama mzazi wa mtoto huyo amesema siku ya tukio hilo mume wake alimpigia simu kuwa mtoto wake wa kike anaumwa vipele sehemu za siri,hivyo alimtaka arudi nyumbani kwa ajili ya uangalizi wa mtoto na ndipo alipobaini kuwa mtoto huyo alifanyiwa unyama huo.

Mama wa mtoto huyo amesema chanzo cha kutofautiana hadi kutengana na mume wake huyo  ni kutokana na tabia ya ulevi  uliyopindukia. 

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, MPONJOLI MWABULAMBO  amethibitisha kumshikilia baba wa mtoto huyo kwa tuhuma za ubakaji na kuwasihi wanawake kuwa karibu na watoto wao pale inapotokea tofauti na wenza wao.

Uhalifu
Maoni