Basi la ABOOD lateketea kwa moto mapema leo, Feb 12,2019

|
Basi la ABOOD lililoteketea kwa moto mapema leo Februari 12, 2019

Basi la abiria la Kampuni ya ABOOD aina ya YUTONG yenye namba za usajili  namba T 877 DJP iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kwenda Morogoro ikiwa na abiria 56 imeteketea kwa moto karibu na maeneo ya Chalinze.

Kamishna Msaidizi mwandamizi  na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Barnabas David Mwakalukwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Akizungumzia ajali hiyo, Kamishna huyo amesema, basi hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva VALERIAN PASCAL BUNDALA mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa Morogoro Mazimbo ambaye inadaiwa kuwa alibaini hitilafu katika mfumo wa umeme wa basi hilo.

Akizungumzia ajali hiyo, Kamishna huyo amesema hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa watu na mali zao huku dereva huyo akishikiliwa na Polisi kwa ajili ya uchunguzi.

Usafiri
Maoni