Binti wa Michael Jackson agoma kumtetea baba yake hadharani

|
Mtoto wa mfalme wa pop wa wakati huo Paris Michael Jackson aliyegomea kumtetea baba yake hadharani

Binti wa marehemu Michael Jackson, Paris Jackson amesema siyo jukumu lake kumtetea baba yake hadharani dhidi ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili za udhalilishaji wa kingono watoto wa kiume.

Binti huyo mwenye miaka 20 amezungumza hayo ikiwa imepita juma moja baada ya kuondoka kwenye makazi ya baba yake ya kifahari yaliyopo Neverland, nchini Marekani kufuatia makala iliyorushwa ikiwaonesha wanaume wawili wakimshutumu marehemu Jackson kuwadhalilisha kingono wakati wakiwa watoto wadogo.

"Sina ninachoweza kusema, ambacho sijawahi kusema kwa ajili ya kumtetea baba yangu hadharani," aliandika katika ukurasa wake wa Twitter binti huyo ambaye kwa sasa ni mwana mitindo.

Ameongeza kuwa anashirikiana na familia yake katika harakati za kulisafisha jina la baba yake huyo aliyekuwa mfalme wa muziki wa Pop nchini Marekani.

Michael Jackson kabla ya kukutwa na umauti aliacha watoto watatu ambao ni Prince, Paris ambao walizaliwa na aliyekuwa nesi wake wa karibu huku Blanket mama yake hakuweza kufahamika.

Maisha
Maoni