BMT yapewa nguvu kisheria kudhibiti michezo ya kulipwa

|
Baraza hili kwa sasa halina mamlaka ya kudhibiti michezo ya kulipwa katika nyanja mbalimbali kama vile ngumi, soka, netiboli, riadha n.k.

Bunge la Tanzania limepitisha mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) inayolitaka baraza hilo kuongezewa nguvu ya kusimamia michezo ya kulipwa kama inavyofanya kwenye michezo ya ridhaa.

Akiwasilisha muswada wa sheria ya mabadiliko ya sheria mbalimbali namba tatu ya Mwaka 2018, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Aderadius Kilangi amesema marekebisho hayo yamelenga kuipa nguvu ya kisheria BMT ili kuweza kudhibiti michezo ya kulipwa.

Kilangi amesema vyama vingi vya michezo ya kulipwa vimekuwa vikikwepa kusajiliwa chini ya sheria ya baraza hilo kwa kisingizio kuwa tafsri ya michezo iliyoko kwenye sheria, inamaanisha michezo ya ridhaa na siyo michezo ya kulipwa.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Uatawala Mohamed Mchengerwa amesema chini ya mabadiliko hayo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali atakuwa na nguvu ya kisheria ya kuingilia kesi yoyote itakayofunguliwa na baraza hilo au dhidi ya baraza hilo.

Michezo
Maoni