Bosi wa EPZA aagizwa kufuatilia kibali cha mwekezaji

|
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa moja ya Kiwanda cha juice mkoani Pwani

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, George Simbakalia afuatilie Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu kibali cha Ujenzi wa Kiwanda cha Nyuzi kinachotakiwa kujengwa Chalinze mkoani Pwani.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mkuu wa Mkoa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo kumuleza kuwa kuna mwekezaji wa Kiwanda cha Kutengeneza Nyuzi cha H and J cha Chalinze ambacho ujenzi wake umekwama kutokana na mwekezaji kutopewa kibali cha ardhi.

Waziri mkuu ametoa agizo hilo leo alipozungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Keda kinachotengeneza marumaru aina ya Twyford kilichopo Chalinze mkoani Pwani pamoja na Kiwanda cha Sayona Fruitti akiwa njiani kwenda jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imedhamiria kuwaunga mkono wawekezaji na kuwafanya wawekeze bila ya urasimu, hivyo amemuagiza kiongozi huyo wa EPZA kuhakikisha kibali kinapatikana.

Viwanda
Maoni