G7 kuchangia elimu ya wasichana maskini

|
Watoto maskini

Canada imesema ina mipango ya kuchangia kiasi cha pauni bilioni 2.9 ikisaidiwa na nchi washirika wa G7 kwa ajili ya kusaidia elimu ya wasichana na wanawake walio maskini.

Fedha hizo zitasaidia kuhakikisha kuwa mpango wa wasichana na wanawake kupata elimu sawa na wavulana na kuwezesha fursa za kujifunza katika nchi mbalimbali duniani, Serikali ya nchi hiyo imeeleza.

Tamko hilo la Jumamosi limekuja kwa kuchelewa kwa kuwa nchi washirika wakiwemo Ujerumani, Japan, Uingereza, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia zilikuwa zikiendelea kuchangia.

Mkutano wa G7 uliofanyika Quebec ni mkutano wa mwaka unaokutanisha nchi za Canada, Marekani, Uingereza, Ufaransa, Italia, Japan na Ujerumani.

Uwekezaji huu unaelezwa kuwa utaweza kuwasaidia watoto na vijana wadogo zaidi ya milioni nane.

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Malala Yousafzai, 20 ameunga mkono zoezi hilo la uchangiaji fedha.

Elimu
Maoni