DART waanza kutafiti namna bora ya kuendesha mradi wa mwendokasi

|
Mabasi ya mwendokasi ambayo sasa Serikali imeamua kuangalia namna bora ya kuendesha biashara hiyo iliyokuwa tegemeo la wengi jijini Dar es Salaam

Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (DART) wamesema wamelazimika kumtafuta mshauri mwelekezi ili afanye utafiti  wa namna bora  ya uendeshaji wa  mradi huo.

Akizungumza na Azam News  Meneja Uhusiano wa DART,  WILLIAM Gatambi amesema wamefikia hatua hiyo ili uendeshaji wa mradi huo uwe na manufaa kwa pande zote mbili  za mwendesha mradi na Serikali.

Kwa mujibu wa Gatambi utafiti huo utakaodumu kwa muda wa miezi mitatu, utaisaidia Serikali kupata suluhu ya kudumu ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto zilizopo kwa sasa katika uendeshaji wake.

Pia Gatambi amebainisha kuwa mtoa huduma aliyepo sasa UDART anaendelea kutoa huduma katika kipindi cha mpito ambacho kilianza mwaka 2016 hivyo baada ya kukamilika kwa utafiti watatangaza zabuni ya kumpata mtoa huduma kamili licha ya hapo awali mwendeshaji kupatikana na kuondolewa baada ya kukiuka vigezo na masharti.

Serikali ilikuja na wazo la kuanzisha mradi wa mabasi ya mwendo wa haraka ikiwa ni moja ya njia ya kuleta suluhu ya kudumu ya msongamano wa magari jijini Dar es salaam.

Usafiri
Maoni