Dereva wa gari la wagonjwa matatani Tarime

|
Mirungi iliyokamatwa ikiwa ndani ya gari la kubeba wagonjwa mkoani Mara

Jeshi la Polisi mkoani Mara limemkatamata mfanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, George Matayi ambaye ni dereva wa gari la wagonjwa  namba DFPA 2955 Toyota Land Cruser linalotumiwa na wilaya hiyo likiwa na viroba 34 vya mirungi vyenye uzito wa kilo zaidi ya 800.

Tukio hilo limetokea leo, Julai 11 katika Kijiji cha Bitaraguru, Kata ya Kibasa wilayani Bunda mkoani Mara.

Dereva huyo amekamatwa na askari wa Jeshi la Polisi akiwa na abiria aliyefahamika kwa jina la Yuda Joseph katika gari ambalo limebeba viroba vya Mirungi kinyume na makusudio ya Serikali kuleta gari hilo.

Kwa mujibu wa Polisi, upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea ili kubaini mtandao wa wahusika wa biashara hiyo.

Uhalifu
Maoni