Dkt. Shein akiri uwepo wa upungufu wa madaktari Bingwa

|
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika Kilele cha Madhimisho ya Mapinduzi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekjiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohammed Shein amesema upungufu wa Madaktari bingwa na wataalamu wa fani ya afya unaathiri utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi visiwani Zanzibar.
 
Aidha Rais Shein amesisitiza kuwa Serikali yake kuanzia Mwezi Julai mwaka huu itarejesha utaratibu wa elimu bure kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari.
 
Dkt. Shein ameyasema hayo leo katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya 54 ya Mapinduzi ya Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani mjini, Unguja.
 
Katika Sherehe hizo maelfu ya wananchi walijitokeza wakiwemo na viongozi wakuu wa nchi, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, pamoja na viongozi wengine wa Bara na visiwani.
 
Aidha Dkt. Shein amesisitiza kuwa serikali yake inazitambua changamoto zote za masuala ya afya na kuahidi kuyatatua likiwemo la madaktari, vifaatiba pamoja na miundombinu.
 
Nao baadhi ya wananchi waliopata wasaa wa kuzungumza na Azam TV, walipongeza mafanikio yaliyofikiwa tangu Mapinduzi, na kusisitiza mshikamano huku wakikemea ubaguzi na matabaka ya Kisiasa.
 
Utawala
Maoni