Dkt. Shein: Saratani ya shingo imekuwa ikiongezeka siku hadi siku

|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein akifuatilia maelekezo ya namna ugonjwa wa saratani unavyoshambulia

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kasi ya maradhi ya saratani ya shingo ya kizazi imekuwa ikiongezeka siku hadi siku hali ambayo imeifanya Serikali kutafakari namna ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Dkt. Shein amesema licha ya idadi hiyo kuongezeka bado wanaopata huduma za matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi ni ndogo kutokana na  gharama za kutibu maradhi hayo kuwa kubwa.

Zaidi ya wanawake 33,000 wanatarajiwa kuchunguzwa maradhi ya saratani ya shingo ya kizazi Kisiwa cha Unguja na Pemba ili Serikali iweze kubaini ukubwa wa tatizo hilo. 

Afya
Maoni