Facebook waifuta akaunti ya gaidi wa New Zealand

|
Gaidi aliyeshambulia misikiti miwili nchini New Zealand ambaye alirusha tukio hilo LIVE kupitia ukurasa wake wa Facebook

Facebook wametekeleza kwa vitendo kwa kuiondoa haraka akaunti ya gaidi muuaji aliyeonesha mbashara shambulio la leo, Ijumaa nchini New Zealand.

Gaidi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Brenton Tarrant, (28), alitumia ukurasa wake wa Facebook kurusha shambulio hilo lililopoteza maisha ya waumini 41 katika msikiti wa Al Noor, huko Christchurch wakati wa maendeleo ya ibada ya Ijumaa.

Inadaiwa kuwa polisi nchini New Zealand waliionya Kampuni hiyo kubwa inayoendesha mitandao ya kijamii, mara tu tukio hilo lilipoanza kurushwa mbashara.

Kutokana na shambulio hilo, Facebook wamethibitisha kutuma salama zao za rambirambi kwa waathirika na familia zao.

Miongoni mwa video zilizoonekana katika tukio hilo ni la gaidi huyo alipokuwa akichukua silaha, ikiwemo bunduki aina ya semi-automatic shotgun na rifle, katika eneo la tukio kabla ya kutoka ndani ya msikiti na kuanza mashambulizi yake hayo ya ‘ukichaa’.

Utawala
Maoni