Filamu inayodaiwa kukosa maadili yafungiwa Kenya

|
Filamu yenye maudhui yalipingwa Kenya

Bodi ya Filamu ya Kenya (KFCB) imeipiga marufuku filamu iitwayo 'Rafiki' inayodaiwa kugusia masuala ya mapenzi ya jinsia moja.

Filamu hiyo ni ya kwanza kutoka Kenya kuchaguliwa ili kuonyeshwa katika Tamasha la Kimataifa la Cannes mwaka huu.

Tamasha la Cannes, ni miongoni mwa matamasha ya filamu makubwa duniani pamoja na Tamasha la Oscars.

Katika matamasha hayo, wachezaji wa filamu, watayarishaji na waongozaji hukutana na  kushindanisha filamu huku nafasi kubwa ya uuzaji filamu ukifanywa na kampuni kubwa.

KFCB imepiga marufuku filamu hiyo kuonyeshwa hadharani au kutangazwa kwenye televisheni ama kusambazwa, ikisema maudhui ya filamu hiyo hayapendezi mbele ya jamii na kwamba yanakiuka sheria za Kenya.

Taarifa ya kupigwa marufuku kwa filamu hiyo ilitolewa na mwandishi na muongozaji wake Wanuri Kahiu kupitia mtandao wao wa kijamii wa Twitter, akisema "ninaamini kuwa watu wazima Kenya wamenyimwa haki zao za kujichagulia maudhui wanayoyataka kuyaona."

Filamu
Maoni