Halima Mdee naye atinga mbele ya Kamati ya Bunge ya Maadili

|
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akiwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Mamlaka ya Bunge kuitikia wito wa Spika wa Bunge

Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee amefika mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge akiitikia wito wa hutuma zinazomkabili za kulilidhalilisha Bunge.

Mdee amefika mbele ya kamati hiyo leo, Jumanne asubuhi katika Ofisi za Bunge mjini Dodoma kama alivyotakiwa kufanya hivyo na Spika, Job Ndugai.

Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee anatuhumiwa kulidhalilisha Bunge baada ya kuunga mkono kauli ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuwa mhimili huo ni dhaifu kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Bunge
Maoni