Hotuba ya Rais Trump yakosolewa

|
Rais Donald Trump wa Marekani

Hotuba ya kitaifa ya Rais Donald Trump wa Marekani imepokewa kwa hisia tofauti huku wachambuzi wa uhakika wa taarifa maarufu kama Facts Checking wakiikosoa hotuba hiyo na kueleza kuwa imejaa taarifa za uongo.

Hii ni hotuba ya kwanza katika Televisheni akilihutumia Taifa,  Rais Donald Trump akatumia fursa hiyo kutangaza mgogoro wa mpakani, akiwalaumu Chama Cha Demokrats kwa kukataa kuidhinisha fedha kwa ajili ya Usalama wa mpaka.

Katika hotuba hiyo Trump anaoekana kuwalaumu Demokrat kwa madai ya kupuuza hali halisi ya jinsi dawa za kulevya zinavyoingia nchini Marekani kupitia mipakani na kwamba mpango wake wa kujenga ukuta katika mpaka wa Mexico kama suluhisho unapingwa na Demokrat.

Trump amekaririwa akisema Mpaka wa Kusini ni njia kuu ya kuingiza dawa za kulevya na kwamba kila wiki Raia 300 wa Marekani hufa kutokana na matumizi ya Heroin pekee na kwamba asilimia 90 ya dawa hizo huingizwa kupitia mpaka huo wa kusini kwa maana ya Mexico.

Hata hivyo wakosoaji wa hotuba hiyo likiwemo Shirika la Habari al Assosiation Press la Marekani wamesema ukweli ukuta wa Trump hauwezi kufanya lolote wakati mzigo mkubwa wa dawa za kulevya unakatwa zaidi katika viwanja vya ndege na siyo katika mipaka ya pembezoni kama alivyoeleza.

Wakosoaji hao pia wamesema ripoti ya 2018, inaonyesha kuwa njia kuu zinazotumika kuingiza kiwango kikubwa cha dawa za kulevya ni kwa kutumia magari ya abiria na katika viwanja vya ndege na bandari, ripoti inayokinzana na hotuba ya Trump.

Utawala
Maoni