H/shauri ya jiji la Mbeya kuijenga Mbeya kwa miaka 20 kuanzia sasa

|
Mnara wa mashujaa uliopo jijini Mbeya

Halmashauri ya jiji la Mbeya imeingia makubaliano na Kampuni ya Kitanzania Urban Solution ambayo itakuwa na jukumu la kuandaa Master Plan ya jiji hilo kwa miaka 20 kuanzia mwaka huu 2019 hadi mwaka 2039 na utatekelezwa katika kipindi cha miezi 18.

Master Plan ya mwisho ilikuwa mwaka 1984 ambayo iliisha muda wake mwaka 2004 na baadaye jiji kujiendesha bila Mpango wowote kwa miaka 15 hali ambayo imechangia kuwepo kwa ujenzi holela.

Mpango huo umefadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia mradi wa uendelezaji miji kimkakati huku kampuni hiyo ikizishinda kampuni nyingine 28 zilizowasilisha maombi ya kushindania zabuni hiyo.

Mazingira
Maoni