Iran kuendelea kukabiliwa na mafuriko zaidi, wengi wahamishwa

|
Wananchi waliozingirwa na maji nchini Iran wakihamishiwa maeneo salama

Iran huenda ikakabiliwa na mafuriko makubwa yatakayoweza kusababisha watu wengi zaidi kuyahama makazi yao kutokana na utabiri kuonyesha kuwa mvua kubwa zaidi inatarajiwa kuendelea kunyesha mwishoni mwa wiki.

Dhoruba kubwa inatarajiwa katika eneo la majimbo ya kusini mwa Irani huku maafisa wa serikali wakitangaza hatua za tahadhari watakazochukua ikiwa ni pamoja na kuruhusu maji kutoka katika kingo za mito ili kupungza kiwango cha madhara ya kuvunjika kwa kingo za mito hiyo.

Wanawake na watoto wamehamishiwa katika maeneo salama huku wanaume wakitakiwa kushiri zoezi la uokozi.

Hadi sasa idadi ya watu waliokufa wamefikia 70, miji kama Susangerd wenye watu 50,000 utakuwa kwenye hatari zaidi na maafisa wamesema watu wanapaswa kuhama mji huo haraka.

Karibia Vijiji 70 watu wake wamehamishwa katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Makampuni ya Nishati katika maeneo yenye utajiri wa mafuta wametumia pampu zao kunyonya na kupunza maji katika maeneo yenye mafuriko.

Mafuriko
Maoni