Iran waadhimisha kumbukumbu ya miaka 40 ya mapinduzi

|
Rais wa Iran, Hassan Rouhani akihutubia maelefu ya WaIran walioadhimisha kumbukumbu ya miaka 40 ya mapinduzi ya Kiislamu.

Raia wa Iran wameandamana nchi nzima kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 40 ya Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.

Sikukuu hii inakuja kukiwa na mvutano kati ya Iran na Umoja wa Mataifa baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuiondoa Marekani kutoka katika mkataba wa nyuklia wa Tehran mwezi Mei mwaka jana na kuiwekea vikwazo vipya Iran mwezi Novemba.

Mamia ya waandamanaji wameonekana leo, Jumatatu katika mitaa ya mjini Tehran na kisha kuhutubiwa na Rais wao, Hassan Rouhani ambaye amesema mapinduzi hayo ni ya kuenziwa muda wote kwa kuwa yameifanya Iran kuondoka mikononi mwa wakoloni.

Pamoja na hayo amesisitiza kuwa wataendelea na mipango yao ya kujihami kwa silaha za kivita dhidi ya maadui zao kwa kuwa hawahitaji kuomba ridhaa ya mtu yeyote kufanya hivyo.

Utawala
Maoni