Jeshi la watu 27 Mtibwa Sugar kuwafuata Washelisheli Jumapili

|
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex, Mtibwa iliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Msafara wa watu 27 wa timu ya Mtibwa Sugar, ukijumuisha wachezaji 18, viongozi sita wa benchi la ufundi na viongozi wawili wa kiutawala, unaondoka kesho Desemba 2, na ndege ya Emirates kuelekea Shelisheli kupitia Dubai.

Wakata Miwa hao wa Manungu Turiani Mkoani Morogoro, wanakwenda Shelisheli kucheza mechi ya mkondo wa pili wa raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya wenyeji wao, Northern Dynamo ambayo itapigwa Desemba 4 mwaka huu.

Mtibwa Sugar inakwenda Shelisheli ikiwa na mtaji mnono wa magoli manne kwa bila iliyopata kwenye mechi ya mkondo wa kwanza Novemba 27 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex ambapo Jaffary Salum Kibaya alifunga mabao matatu (Hat-Trick) na Riphat Khamis Msuya akafunga goli moja.

Ili isonge mbele, Mtibwa Sugar itahitaji ushindi wowote ule au kufungwa si zaidi ya magoli 3-0, jambo ambalo linaonekana litakuwa gumu kutokana na kiwango cha kawaida walichoonesha Northern Dynamo kwenye mechi wa kwanza.

CAF
Maoni