Jiji la Dar es Salaam sasa kuongozwa na manaibu meya wawili

|
Manaibu meya wa Jiji la Dar es Salaam, watakaoongoza kwa kupokezana baada ya kugongana kwa kura

Hatimaye Jiji la Dar es Salaam, limefanikiwa kupata manaibu Meya wawili baada ya wagombea wawili kugongana kwa kupata kura 12/12.

Wawili hao waliogongana kura hizo baada ya kurudiwa mara kadhaa ni pamoja na mgombea wa CCM, Mariam Lulida, Diwani wa Kata ya Mchafukoge na Ally Harubu wa Kata ya Makumbusho kwa tiketi ya Chama cha CUF, ambao kutokana na kufungana huko, sasa wataongoza kwa kupokezana kwa miezi mitatu mitatu kuanzia Disemba 30.

Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam na hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa mkutano huo kufikia uamuzi huo na wawili hao wanachukua nafasi ya Mussa Kafana aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kilawi CUF.

Siasa
Maoni