Kesi ya kina Zitto na wenzake yaanza kusikilizwa Mahakama Kuu

|
Kiongozi wa ACT -Wazalendo, Zitto Kabwe akiwa mahakama kuu na wenzake waliofungua kesi kupinga muswada wa mabadiliko ya sheria ya vyama vya siasa nchini

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeanza kusikiliza kesi ya kupingwa Muswada wa marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa iliyowasilishwa na wanasiasa, Zitto Kabwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, pamoja na wanachama wa Chama cha Wananchi CUF,  Joran Bashange na Salum Bimani.

Kesi hiyo imeendelea kusikilizwa leo mahakamani hapo kwa pingamizi la Serikali dhidi ya shauri namba 31 la mwaka 2018 la kupingwa kwa muswada huo.

Mahakama Kuu imesitisha usikilizwaji wa shauri la msingi ili kusikiliza kwanza pingamizi la upande wa Serikali ambao wanaitaka mahakama hiyo itupilie mbali ombi la Zitto Kabwe na wenzake.

Mawakili wa Serikali wameijulisha Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo kuwa wana hoja Kumi za kulipinga shauri la msingi.

Mahakamani
Maoni