Kesi ya kupinga matokeo DR Congo yaendelea

|
Mgombea wa urais na mshindi wa pili wa uchaguzi nchini DR Congo, Martin Fayulu akiwa mahakamani

Mahakama ya Katiba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaendelea kusikiliza malalamiko dhidi ya matokeo ya uchaguzi yaliyopingwa ambayo yalimpatia ushindi kiongozi wa upinzani, Felix Tshisekedi.

Mahakama hiyo iliyoanza kusikiliza malalamiko ya Martin Fayulu aliyedaiwa matokeo hayo ya uchaguzi kuwa ni batili imeendelea kusikiliza hoja mbalimbali huku wananchi wa nchi hiyo iliyotawaliwa kwa kipindi kirefu na Rais Joseph Kabila wakisubiria kwa hamu uamuzi huo.

Matokeo ya awali ya uchaguzi yalimpatia Felix Tshisekedi asilimia 38.57 ya kura dhidi ya asilimia 34.8 za Martin Fayulu, Mgombea anayeungwa mkono na Rais Joseph Kabila, Emmanuel Ramazani Shadary alishika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 23.8.

Mahakamani
Maoni