Kiboksi cha kurekodi taarifa za ndege iliyoanguka chapatikana

|
Eneo lilipoangukia mkia ambapo kifaa maalum cha kurekodi taarifa za mwenendo wa ndege iliyoanguka kilipopatikana

Wachunguzi wamefanikiwa kukipata chombo maalum cha kurekodi taarifa za mwenendo wa ndege  maarufu black box cha ndege ya Shirika la Ethiopia iliyoanguka jana, Jumapili muda mfupi baada ya kuruka.

Vifaa hivyo vya kurekodi sauti na taarifa za kidigitali za ndege vilipatikana katika eneo ulipoangukia mkia wa ndege hiyo aina ya Boeing 737 Max 8.

Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Addis Ababa kwenda Nairobi, Kenya, ambapo ilianguka ndani ya dakika sita baada ya kupaa na kuua watu wote 157 waliokuwa ndani ya ndege.

Ndege kadhaa zenye muundo wa ndege hiyo zimezuiwa kusafiri kufuatia tukio hilo la kutisha.

Ndege hiyo ilianguka karibu na mji wa Bishoftu, kilomita 60 sawa na maili 37 kusini – mashariki mwa mji wa mkuu wa Addis Ababa ina miezi kadhaa tangu inunuliwe.

Inadaiwa kuwa na abiria kutoka mataifa zaidi ya 30, wakiwemo Wakenya, Waethiopia, Wacanada na Waingereza.

Maisha
Maoni