Kiongozi Korea Kaskazini azuru China

|
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un akiwasili nchini China akiwa ameambatana na mkewe Ri Sol-ju

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amewasili jijini Beijing, kwa ziara ambayo haikutangazwa rasmi, ikiwa ni mwaliko wa Rais wa China, Xi Jinping.

Kim anatarajiwa kuwepo nchini humo hadi Januari 10 akiwa ameambatana na mkewe Ri Sol-ju, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.

Ziara hiyo imekuja huku kukiwa na taarifa za kuendelea kufanyika kwa majadiliano yatakayohusu mkutano wa pili kati ya Kim na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Wawili hao awali walikutana mwezi Juni mwaka jana katika mkutano wa kipekee kwa Rais wa Marekani.

Utawala
Maoni