Kiongozi wa upinzani Venezuela aitisha maandano mapya

|
Maelfu ya waandamanaji nchini Venezuela wakiwa katika maandamano yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani, Juan Guaido

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Juan Guaido, ameitisha maandamano mapya ikiwa ni siku ya 50 tangu kuwapo kwa mzozo wa kisiasa ulioathiri pakubwa shughuli za serikali nchini humo.

Waandamanaji wenye hasira iliyochanganyika na matumani ya kupata wanachotaka, walibeba mabango yanayomtaka Maduro kuondoka madarakani.

Maandamano haya yanakuja wakati ambapo mwendesha mashitaka wa serikali akipanga kufanya uchunguzi na kisha kufungua mashtaka dhidi ya Guaido akituhumiwa kuhujumu mfumo wa umeme nchini humo.

Hii ni itakuwa hatua nyingine kuchukuliwa na serikali dhidi ya kiongozi huyo wa upinzani anayeungwa mkono na mataifa hamsini ikiwemo Marekani baada ya kurejea Venezuela wiki iliyopita akidaiwa kupuuza zuio la kusafiri alilowekewa na serikali ya Maduro.

Utawala
Maoni