Kyerwa kumalizia ujenzi wa zahanati ilikwamba kwa miaka 10

|
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali, Marco Gaguti akishiriki ujenzi wa zahanati iliyokwama kwa miaka 10

Wakazi wa Kijiji cha Chanya wilayani Kyerwa mkoani Kagera wameanza jitihada za kumalizia ujenzi wa zahanati iliyokwama zaidi ya miaka 10 ili  kuondokana na adha ya  kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 15 kutafuta huduma ya matibabu.

Zahanati hiyo ambayo ilianzwa kujengwa kwa nguvu za wananchi  mwaka 2008, ujenzi wake ulisimama kutokana na ukosefu wa fedha jambo ambalo liliendelea kuwafanya wananchi kutumia gharama kubwa kufuata huduma za matibabu katika hospitali na vituo vya afya vilivyo mbali na kijiji hicho.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, Kashunju Runyogote amewataka wananchi kuongeza jitihada za ukamilishaji wa jengo hilo ambalo amedai lilikwama kutokana na baadhi ya wanasiasa kuwazuia wananchi wasiendelee kutoa michango kwa ajili ya kulimalizia.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali, Marco Gaguti ameunga mkono juhudi za wananchi hao za kumalizia ujenzi wa zahanati hiyo kwa kutoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 na kumuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika ndani ya miezi miwili na inaanza kutoa huduma kwa wananchi.

Afya
Maoni