Lukuvi awapasha watendaji wa Ikwiriri

|
Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi, William Lukuvi akizungumza na wananchi na watendaji wa Ikwiriri, Rufiji

Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi, William Lukuvi ambaye yuko katika ziara ya kikazi wilayani Rufiji ametembelea Kijiji Cha Namwage na Ikwiriri kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo hayo leo, Jumanne.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikwiriri, kuhusu malalamiko ya kuwepo kwa uuzaji ardhi kiholela unaofanywa na watendaji wa vijiji, Waziri Lukuvi amewaambia wananchi hao kuwa mwenye mamlaka ya kutangaza matumizi ya ardhi kuanzia ekari 50 ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Lukuvi pia aliwaasa wananchi hao na watendaji kuacha vurugu zisizo na tija  ambazo haziwasaidi kitu na badala yake zinarudisha nyuma maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mohamed Mchengerwa kwa upande wake amewasisitiza wananchi wake kuhusu kulima na kupanda mazao ya chakula na biashara katika maeneo yao badala ya kuyaacha wazi na kukemea mabishano yasio na tija miongoni mwao.

Utawala
Maoni