Maalum Seif Sharif Hamad ajiunga rasmi ACT WAZALENDO

|
Maalim Seif Sharif Hamad aliyetangaza kuhamia Chama cha ACT WAZALENDO leo na kukihama Chama cha Wananchi CUF
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, viongozi na wanachama wengine wanaomuunga mkono ndani ya chama hicho, wametangaza kujiunga na Chama cha ACT-Wazalendo.
 
Maalim Seif kupitia MCL Digital amesema, walichoamua leo ni kuandika historia mpya ya mabadiliko ya kisiasa kwa Tanzania Bara na Visiwani kwani Umma haujawahi kushindwa popote duniani.
 
Maalimu Seif amesema, wameamua kulitumia Jahazi la ACT WAZALENDO ili kuleta demokrasia, kusimamia haki, utu na ubinadamu na yenye neema inayowafikia watu wote na hawana wasiwasi kwamba watashinda.
 
Amemalizia kwa kusema, " wakati ni huu, wakati ni sasa, shusha tanga, pandisha tanga safari iendelee." alimalizia kiongozi huyo aliyetangaza rasmi kujiunga na ACT WAZALENDO na kuachana na CUF.
 
Kuhusu kwanini amefikia uamuzi huo wa kujiunga na  ACT WAZALENDO na si vyama vingine, Maalim Seif amesema kabla ya uamuzi huo walitembelea vyama vingine na kuhoji masharti waliyopewa na kuyachambua na kisha kuamua kujiunga na chama hicho ambacho kilikuwa na masharti mepesi
 
Kuhusu kunyang'anywa kwa mali za CUF, kiongozi huyo amesema hawana haja navyo na wameamua kusonga mbele huku akikiri kupoteza muda wake mwingi katika kukijenga chama hicho na kukanusha kuhusu shutuma za kukinunua Chama cha ACT WAZALENDO na kusema ni uzushi ulioanzishwa na waliofilisika kimawazo.
Siasa
Maoni