Mabingwa wa El Clasico Super Bonanza wadaka ving’amuzi

|
Mabingwa wa El Clasico Super Bonanza, timu ya Barcelona ya Vingunguti walipokabidhwa ving'amuzi vya Azam TV na Muwakilishi wa La Liga Tanzania Luis Cardenas ndani ya studio za Azam TV.

Azam Media kwa kushirikiana na Ligi Kuu ya Hispania #LaLigaSantanderwamekabidhi zawadi ya ving'amuzi vya #AzamTV kwa timu ya Barcelona ya Vingunguti jijini Dar es Salaam baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa katika Bonanza la #ElClasico ( #ElClassicoSuperBonanza ) lililofanyika Machi 2, mwaka huu kwenye viwanja vya JMK Youth Park Dar es Salaam.

Waliokabidhi zawadi hizo ni mwakilishi wa #LaLiga hapa nchini, Luis Cardenas akiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Azam Media, Abdul Mohamed, tukio likifanyika ndani ya studio za Azam TV.

Bonanza hilo lilizikutanisha timu za Barcelona na Real Madrid kutoka maeneo mbalimbali nchini ambapo Barcelona ya Vingunguti iliibuka na ubingwa.

Soka Tanzania
Maoni