Macron: Nimemshawishi Trump kutoondoa vikosi vya Marekani Syria

|
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amesema, amemshawishi Rais wa Marekani, Donald Trump kutoondoa vikosi vya majeshi yake, nchini Syria na badala yake “ wajipange kukaa hapo kwa muda mrefu zaidi”.

Mapema mwezi huu, Rais Trump alitangaza kuwa Marekani inatarajia "kuondoka nchini Syria haraka".

Hata hivyo, mwishoni mwa Juma, nchi za Marekani, Uingereza na Ufaransa walipiga maeneo muhimu ya serikali ya Syria kwa kile walichokiita ni kujibu mashambulizi kufuatia shambulio la sumu linalotuhumiwa kufanywa na serikali hiyo katika eneo linalokaliwa na waasi.

Rais Macron amesema pia amemshauri Rais Trump kufanya mashambulio kwa kiasi.

Wawili hao, wanaodaiwa kuwa  katika uhusiano wa kirafiki  hivi karibuni, wamekuwa wakizungumza mara kadhaa kabla ya kufikia uamuzi wa kushambulia Syria.

Lakini hata hivyo, mara baada ya Macron kusema hayo, Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Sarah Sanders amesema: "Mipango ya Marekani hajabadilika na Rais Trump analijua hilo kuwa vikosi vya Marekani vinatakiwa kurejea nyumbani haraka iwezekanavyo".

Utawala
Maoni