Madini ya Ruby Longido yazua hofu ya mapigano

|
Waziri wa Madini, Angela Kairuki akitoa maelekezo kwa wamiliki wa migodi ya madini ya Ruby wanaosigana

Shughuli za uchimbaji wa madini ya Ruby kwenye migodi iliyopo Kijiji cha Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha zimeingia dosari baada ya kujitokeza kwa muingiliano wa chini ya ardhi baina ya Kampuni mbili za Mundarara na Sendeu Mining.

Suala hilo limeibua hofu ya kujitokeza kwa mapigano baina ya wachimbaji hao baada ya kuripotiwa kwa matukio kadhaa ya kutishiana silaha za moto kufuatia mgongano huo wa chini ya ardhi unaofahamika zaidi kwa jina la (MTOBOZANO).

Mgodi wa Mundarara Mining unamilikiwa na Mfanyabiashara Rahim Molle huku ule wa Sendeu ukiwa chini ya Lekule Laiser ambaye alikuwa ni mbunge wa Longido na mwenyekiti mstaafu wa CCM wa Mkoa wa Arusha.

Waziri wa Madini, Angela Kairuki amezuru kwenye eneo hilo na kuzitaka pande zote mbili kukaa pamoja na wataalamu wa wizara yake kuona njia za kusuluhisha mgogoro huo na ikiwa itashindikana Serikali itachukua hatua za kuifunga migodi hiyo mara moja.

Madini
Maoni