Madiwani wakubaliana kufanyia marekebisho mnara wa GEITA

|
Mnara wa Mji wa Geita ambao ulileta taharuki baada ya kutambulishwa rasmi

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Geita kwa pamoja limeazimia kuufanyia ukarabati mnara ulioko katikati ya mji wa Geita uliojengwa  kwa thamani ya shilingi milioni 70 na kukamilika mwezi mmoja uliyopita.

Mnara huo uliojengwa kwa fedha zilizotokana na malipo ya mahusiano ya mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) umelalamikiwa na wadau mbalimbali kuwa na mapungufu kadhaa ikiwa maandishi mengi yanayoonyesha nembo za GGM na kutokuwa na nembo maalum inayowakilisha uhalisia na uwakilishi wa Mkoa wa Geita.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita amesema kuwa, ukarabati huo unafanyika ili kuondoa alama zote zinazoonyesha umiliki wa mnara na kuweka uhalisia wa Geita yenyewe.

Madiwani hao wameazimia kukarabati mnara huo kwa gharama ya zaidi ya milioni tano (5) ili kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi  wa mji wa  Geita, John John amesema kuwa bajeti ya kukarabati mnara huo haitazidi milioni tano na kuongeza kuwa fedha za ujenzi wa awali zilitokana na fedha za mahusiano kutoka mgodi wa GGM(CSR).

Utawala
Maoni